Ndaki ya kilimo yashiriki uzinduzi wa agenda za utafiti wa mifugo, uvuvi na ukuzaji wa viumbe maji

uzinduzi ajenda ya kitaifa ya mifugo na uvuvi CoA

Siku ya Jumamosi tarehe 16 Novemba 2019, Ndaki ya Kilimo ilishiriki uzinduzi wa agenda za utafiti wa mifugo, uvuvi na ukuzaji wa viumbe maji uliofanyika katika kamapasi ya Solomon Mahlangu, iliyopo Mazimbu, Morogoro.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina (MB) alizindua agenda hizo na kueleza malengo yake ikiwa ni pamoja na

  1. kuzifungua tafiti zilizofanyika miaka ya nyuma na kuzifikisha kwa watumiaji
  2. kuweka utaratibu wa kutambua, kuorodhesha na kutumia tafiti zinazofanywa na wanafunzi wa shahada za uzamili
  3. kuweka kanuni zinazotoa muongozo wa utekelezaji wa agenda na kuhakikisha watafiti wanatekeleza wajibu wao na
  4. kuweka utaratibu wa kuwaunganisha watafiti wa mifugo na uvuvi. Agenda hizi pia zinalenga kuweka msingi wa kusimamia watafiti kufuatana na mahitaji ya soko na mambo muhimu kitaifa pamoja na kuongeza mnyororo wa thamani kwenye bidhaa za mifugo na uvuvi.

Awali Mh. Mpina alisema anatambua SUA kuwa kiungo muhimu cha shughuli za mifugo na uvuvi . Kwa upande wake Makamu wa Mkuu wa Chuo prof. Raphael Chibunda aliishukuru Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuchagua SUA kuwa sehemu ya kuzindua agenda hizo. Ndaki ya Kilimo iliiwakilisha SUA kwenye kamati ya maandalizi chini ya Prof. Sebastian Chenyambuga

uzinduzi ajenda ya kitaifa ya mifugo na uvuvi CoA

Related Posts