IDARA YASHIRIKI KONGAMANO LA KILIMO MIAKA 63 YA UHURU

Tarehe 6, Disemba idara ya sayansi ya mimea,vipando na mazao ya bustani ilishiriki kongamano la miaka 63 ya Uhuru liliondaliwa na menejimenti ya Chuo  likijadili Kilimo tulipotoka ,tulipo na mustakabali wa Tanzania Bora.

Kupitia mwakilishi wake Dr.Yasinta Nzogela Mhadhiri na mbobezi wa kilimo ambaye  alitoa mchango wake na kuelezea maendelo ya teknolojia na uzalishaji wa mazao ya kilimo.Katika kuchangia Dr.Yasinta alisisitiza umuhimu wa tafiti na uwezeshwaji wakulima kwa mbegu bora na pembejeo za kisasa.Aidha alisema kwa sasa kama Taifa tumefanikiwa kuzalisha chakula cha kutosha na mazao ya kibiashara hali inayokuza na kufungua soko la mazao nje ya Tanzania.Pia alisisitiza kwamba mnyororo wa thamani wa kilimo ni mkubwa na hivyo  ni fursa kwa vijana kushiriki na kujitoa ili kuchochea maendeleo ya sekta hiyo.

 

Dr.Yasinta Nzogela,Mhadhiri kutoka idara ya sayansi ya mimea,vipando na mazao ya bustani.

Kongamano hili lilihudhuriwa na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali mkoani Morogoro,walimu na wafanyakazi wa SUA.Idara inapongeza menejimenti ya chuo kwa kuandaa kongamano hili na kutumia wataalamu mbalimbali katika idara kutoa elimu na Mawazo ya kisayansi kwa maendeleo