Mnamo tarehe 07/03/2024 wana CDA walitumia jukwaa la redio kutoa elimu kuhusu haki za mwanamke kupitia kipindi Cha redio Cha ZOE FM. Kwa ustadi na weledi, waliweza kufafanua kwa kina masuala muhimu yanayohusu haki za wanawake na kuchangia katika kujenga jamii yenye usawa na haki.
Kipindi hicho kilileta faida kubwa kwa jamii. Kwanza, kilichochea uelewa mpana kuhusu haki za mwanamke, kikiwasilisha maelezo kwa lugha rahisi na inayoeleweka. Pili, walisaidia kubomoa mithili na imani potofu zinazohusu haki za wanawake, wakionyesha umuhimu wa usawa na haki kwa maendeleo ya kijamii.
Zaidi ya hayo, kipindi hicho kilikuwa daraja la kuwapa wanawake sauti na nafasi ya kushiriki kikamilifu katika mijadala inayohusu haki zao. Kwa kufanya hivyo, wana CDA wameonyesha jinsi wanavyotilia maanani ushirikishwaji wa jamii na kuelimisha kwa njia endelevu. Jitihada hii imeimarisha uwepo wa wanawake katika kuchangia maamuzi na kujenga jamii yenye haki na usawa.
“It’s possible….”