Shiriki Katika Maadhimisho Ya Siku Ya Ukimwi Duniani

Siku ya tarehe 01/12/2022, viongozi pamoja na wanachama wa Asasi Ya Jumuiya Ya Maendeleo Ya Jamii (Community Development Association CDA) walishiriki katika maadhimisho ya siku ya UKIMWI duniani yaliyofanyika katika viwanja vya chuo cha mifugo liti Manispaa ya Morogoro. Ikiwa ni baada ya kupoke mwaliko kutoka Halimashauri ya Manispaa ya Morogoro. Maadhimisho hayo yalitanguliwa na maandamano yaliyoanzia katika ofisi za kata ya Mji Mkuu hadi uwanja wa liti. Aidha katika maadhimisho hayo CDA ilipata nafasi ya kutoa mada juu ya UKATILI WA WANAWAKE NA WATOTO na maambukizi ya UKIMWI. Wakizungumza katika maadhimisho hayo watoa mada kutoka CDA Rose Machibya na Aziza Gwabara wametoa wito kwa jamii juu ya ukatili wa wanawake na watoto kwa kuwahimiza kuzingatia sheria zilizowekwa juu ya ukatili, kuboresha huduma za uzazi salama na kupaza sauti pale matukio ya ukatili yanapotokea ili kupunguza na kuondoa kabisa tatizo hili kubwa la ukatili.

Share this

Related Posts