Tukio la Kijamii

Siku ya tarehe 28-01-2023, wanafunzi wanaosoma shahada ya Maendeleo ya jamii kupitia Asasi ya Maendeleo ya Jamii (CDA) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine Cha Kilimo (SUA), Kwakuonesha udhamini wao katika jamii, walitembelea kaya zinazoishi katika mazingira magumu katika Kata ya Magadu. Lengo ikiwa nikuwasaidia na kupanda miche ya matunda (Maembe) ambapo kila kaya iliweza kupandiwa miche mitano (5) na kupewa msaada wa chakula.
Wananchi wa kata ya Magadu walilipokea jambo hili kwa mtazamo chanya kwani walihitaji msaada zaidi kutoka kwa wana asasi, hivyo CDA kwa kuliona hilo imepanga kufanya jambo hili la kutembelea kaya zinazoishi katika mazingira magumu kuwa endelevu kwa misingi ifuatayo;
1. Kuunda vikundi vya hizi kaya zinazoishi katika mazingira magumu na kuvisimamia ili iwe rahisi kukutana nao pindi wana asasi watakapo wahitaji pia itasaidia wao wenyewe kuweza kujisaidia.
2. Kuwajengea uwezo wa katika kilimo biashara pamoja na  ujasiriamali ili waweze kufanya biashara ndogo ndogo zitakazowaingizia kipato cha kujikwamua na maisha yao.
Mwisho, uongozi wa asasi ya Maendeleo ya jamii CDA inapenda kutoa shukrani za dhati kwa idara ya Ugani na Maendeleo ya jamii ,kipekee uongozi wa CDA unatoa shukrani kwa Makamu mkuu wa chuo *Profesa Rafael Chibunda* kwa kutoa ruhusa kwa Wanafunzi kuweza kuwa sehemu ya kuisaidia Jamii inayozunguka eneo la chuo ili iweze kunufaika. Jamii ni jukumu letu sote tunapaswa kushirikiana ili kuleta maendeleo chanya katika jamii zetu
“IT’S POSSIBLE, MAKE IT HAPPEN”
Share this

Related Posts