Ushiriki katika maadhimisho ya siku ya mwanamke

Mnamo tareh 08/03/2024, wana CDA wameshiriki kikamilifu katika maadhimisho ya Sikukuu ya Wanawake Duniani, tukio lenye mvuto na matukio mengi yaliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi kiwanja Cha ndege. Kwa shauku na hamasa, wamechukua jukumu la kubeba mabango yenye jumbe za kuvutia, yaliyoleta msisimko na kuonyesha mshikamano wao.
Shughuli za maonesho zimekuwa dira ya ubunifu wa wana CDA katika maeneo ya sanaa, ufundi, na miradi ya maendeleo. Mabango yenye ujumbe wa kuvutia yamechagizwa na ujasiri wao, yakisisitiza umuhimu wa mchango wa wanawake katika ujenzi wa jamii imara na endelevu.
Faida kubwa ya tukio hili ni kuchagiza uelewa na kusherehekea mafanikio ya wanawake katika jamii. Kupitia michoro ya kisanii na ujumbe wa mabango, wamefanikiwa kuhamasisha mjadala na kujenga umoja katika kuleta mabadiliko chanya. Maadhimisho haya yamekuwa ni fursa nzuri ya kuenzi na kuthamini mchango wa wanawake katika kuleta maendeleo.
“It’s possible…..”
May be an image of 8 people and text
Share this

Related Posts