Viongozi wa taasisi ya Maendeleo ya Jamii iwametembelea ofisi za Morogoro Paralegal

Viongozi wa taasisi ya Maendeleo ya Jamii inayoendeshwa na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine mkoani Morogoro wametembelea ofisi za Morogoro Paralegal ambapo pamoja na mambo mengine wamethibitisha kushiriki kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Wadau wa Morogoro Paralegal tarehe 28.06.2024 utakaofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Savoy.

Mbali na ushiriki wao kwenye jukwaa la wadau wa MPLC viongozi hao wamemuomba Mkurugenzi Mtendaji wa Morogoro Paralegal ndugu Amani Mwaipaja kuwa tayari kuwasaidia katika kuwajengea uwezo ili waweze kutimiza malengo ya kuanzisha taasisi yao hiyo ya wanafunzi.

Mkurugenzi wa MPLC ameahidi kuwapa ushirikiano viongozi hao pamoja na wanachama wake na kutoa wito kwa taasisi,vikundi na mashirika yasiyo ya kiserikali kushirikiana kwa karibu na MPLC ili waweze kupeana uzoefu katika uendeshaji wa mashirika yasiyo ya kiserikali katika kuhudumia jamii ya watanzania.

Ndugu Amani Mwaipaja amesema Morogoro Paralegal Centre ina uzoefu wa zaidi ya miaka 30 tangu lilipoanzishwa mwaka 1993

 

 

Related Posts