IDARA YA SHAMBA LA MAFUNZO SUA “MTF” YASHIRIKIANA NA “SUGECO” KUTOA MAFUNZO YA VITENDO KWA WANAFUNZI JUU YA KILIMO HIFADHI CHA KIBIASHARA.

IDARA YA SHAMBA LA MAFUNZO SUA “MTF” YASHIRIKIANA NA “SUGECO” KUTOA MAFUNZO YA VITENDO KWA WANAFUNZI JUU YA KILIMO HIFADHI CHA KIBIASHARA.
Shamba la mafunzo SUA kwa kushirikiana na “Sokoine University Graduate Entrepreneurs Cooperative (SUGECO)”wameendesha kwa Pamoja mafunzo ya kilimo hifadhi cha kibiashara kwa wanafunzi yaliyojumuisha namna bora ya uzalishaji, kilimo biashara na utunzaji wa mazingira.,sanjari na hayo wanafunzi walipata wasaa wa kufahamu namna ya kuhifadhi maji kwaajili ya umwagiliaji ikiwa ni nguzo kuu ya mapinduzi ya kiikolojia katika uzalishaji ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa maji katika uzalishaji hali itakayosaidia uzalishaji wenye tija.

Wanafunzi wakijifunza uhifadhi wa maji katika bwawa la kuhifadhia maji lililopo kituoni SUGECO
Wanafunzi walipata wasaa wa kujifunza kilimo cha kitalu nyumba na faida zake, ambazo ni pamoja na kuzalisha mazao mengi katika eneo dogo,kudhibiti visumbufu vya mimea na hali ya hewa hivyo kupunguza matumizi ya viuatilifu., pia wanafunzi walijifunza mazao stahiki kuzalishwa katika kitalu nyumba ambayo ni mazao yenye thamani kubwa sokoni ili kurudisha gharama za ujenzi wa kitalu nyumba kwa wepesi na kutengeneza faida ikiwa ni sehemu ya mlengo wa kuzalisha kibiashara.

Mwakilishi kutoka SUGECO akitoa ufafanuzi juu ya uzalishaji katika kitalu nyumba
Imeandaliwa
Idara ya Shamba la Mafunzo
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo
0766348077

Related Posts