Ni takribani wiki sita sasa tangu kituo cha bustani mboga mboga na matunda (horticulture unit) kipokee wanafunzi wa kozi mbalimbali ka kilimo kama (agriculture general, horticulture, applied agricultura extensioan) ambao walishiriki mafunzo kwa vitendo kwa muda wa wiki tano kwa ajili ya kupata ujuzi na maarifa kuhusi mambo ya bustani, mbogamboga, matunda Pamoja na viungo.Moja ya utaalamu na ujuzi walioupata ni juu ya kilimo cha Iliki (cardamom) moja ya kiungo kinachopatikana katika kituo cha bustani ,mbogamboga na matunda (horticulture unit).
Iliki ni kiungo ambacho hutumiwa katika upishi wa nchi nyingi za Asia, Afrika, Ulaya na hata Amerika. iliki ni moja kati ya mazao ambayo yanatumika sana karibia kila siku kwenye matumizi ya nyumbani,utumika kama viungo kwenye chakula na pia utumika kama tiba ya magonjwa mbalimbali.na pia ni mmea mfupi ambao unatoa matunda kwa miaka mingi.
Kuna njia mbili za kuotesha iliki unaweza kupanda mbegu au ukapanda miche midogo(spilits)sia mbegu kwenye kitalu baadae kuihamishia shambani
- Wanafunzi hao walishiriki kuhamisha miche ya Iriki kutoka kwenye viliba (polythene bags) na kuipanda shambani kwa ajili ya kuendeleza ukuaji na hatimaye kupata zao la mwisho.
Miche ya iriki inapatika na kuuzwa katika shamba la mafunzo la mfano katika kituo cha bustani mbogamboga na matunda (horticulture unit) Kilichopo Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo (Sua).
Andiko limeandaliwa na;
Simon mayenga setta
0759924182