UVUNAJI WA SAMAKI AINA YA SATO NA KAMBALE

Tarehe 25 Aprili 2024, wanafunzi wa Shahada ya Sayansi ya Ufugaji Viumbe Maji, wakiwa Idara ya Shamba la Mfano la Mafunzo (Kitengo cha Ufugaji wa Samaki) wakionyesha umahiri wao kwa vitendo walipokuwa wakifanya zoezi la uvunaji wa samaki aina ya Sato na Kambale.

Uvunaji huu wa samaki ulihusisha mchakato wa kuwatenganisha samaki katika makundi mawili makuu: wale ambao wamefikia ukubwa unaofaa kwa ajili ya kwenda sokoni, na wale ambao bado wanahitaji muda zaidi wa kukua.

Hatua hii ni maandalizi muhimu kuelekea uuzaji wa samaki kwa jamii. Kwa sasa, Idara ya Shamba la Mfano la Mafunzo-SUA inajiandaa kwa uuzaji wa samaki hao kwa wanajamii. Hivyo, tunaomba watu wote wajiandae kufurahia fursa hii adimu ya kupata samaki safi na bora, moja kwa moja kutoka kwenye Kitengo cha Ufugaji wa Samaki.

Tutatoa taarifa zaidi kuhusu tarehe na taratibu za uuzaji hivi karibuni kupitia Kitengo cha Mawasiliano na Masoko-SUA. Kwa sasa, tafadhali jiandae kwa kununua samaki wa ubora kutoka kwetu!

Kwa Maulizo, Tafadhali Wasiliana Na:

Meneja wa Kitengo: 

Jina: Stella Genge

Barua Pepe: stella.genge@sua.ac.tz

Simu Na: +255-712-413-590

 

Field Technician:

Jina: Buharata Salum

Barua Pepe: buharata.salum@sua.ac.tz

Simu Na: +255-747-612-361

 

Kwa Mawasiliano ya Kiofisi, Tafadhali Wasiliana Na: 

Mkuu wa Idara, Shamba la Mfano la Mafunzo,

Chuo cha Sokoine cha Kilimo (SUA),

S.L.P 3001, Chuo Kikuu, Morogoro,

Simu Na: +255753937587

Barua Pepe: newtonk78@sua.ac.tz  

CC: dmtf@sua.ac.tz

 

Related Posts