WAFANYAKAZI KUTOKA BENKI MBALIMBALI NCHINI WAPATA MWANGA KATIKA UFUGAJI WA SAMAKI KIBIASHARA
Tarehe 18 Aprili, 2024, Wafanyakazi kutoka benki za Exim bank, TPB, DTB na Mkombozi walifanya ziara ya kipekee katika Kitengo cha Ufugaji wa Viumbe Maji kilichopo katika Idara ya Shamba la Mfano la Mafunzo katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA).
Wafanyakazi hawa walishuhudia teknolojia za kisasa zinazotumiwa katika ufugaji wa samaki aina ya Sato na Kambale. Lengo kuu la ziara yao lilikuwa ni kujifunza na kufahamu mbinu za kuwekeza kwenye ufugaji wa samaki kibiashara.
Wafanyakazi hawa, ambao wengi wao wanakaribia kustaafu, walipata fursa adimu ya kujifunza mbinu za uzalishaji wa vyakula vya asili vya samaki kama vile Inzi chuma, Azola, na Minyoo wekundu. Aidha, walishuhudia uzalishaji na ufugaji wa vifaranga vya Kambale na Sato, pamoja na mfumo wa kisasa wa kufuga samaki kwa kutumia mzunguko wa maji (RAS/Recirculating Aquaculture System) na mabwawa mbalimbali yaliyojengwa kisasa.
Mmoja wa wafanyakazi hao alitoa maoni yake kwa kusema:
__“Ni dhahiri kuwa Kitengo cha Ufugaji wa Viumbe Maji-SUA ni mabingwa wa kweli katika ufugaji wa samaki kibiashara. Wenzangu wanapaswa kufika hapa na kujifunza kwa vitendo ili waweze kuongeza mapato yao.”_
_
Hatimaye, tunawakaribisha wafanyakazi na wadau wote kutoka maeneo mengine kujifunza zaidi kuhusu ufugaji wa samaki kibiashara kwa kutembelea Shamba la Mfano la Mafunzo-SUA.
Mawasiliano:
Mkuu wa Idara Shamba la Mfano la Mafunzo | +255753937587 | newtonk78@sua.ac.tz
Meneja Kitengo cha Ufugaji wa Viumbe Maji | +255712413590