Tarehe 21 Mei 2024, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Prof. Raphael Chibunda, aliambatana na Ndugu, Fadhil Maganya, Mwenyekiti wa Taifa Umoja wa Wazazi Tanzania “Jumuiya ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)” na Mjumbe wa Kamati Kuu, walipotembelea Shamba la Mfano la Mafunzo (Model Training Farm), Kitengo cha Ufugaji Viumbe Maji (Aquaculture Unit-SUA). Ndugu Fadhil Maganya (wapili kutoka kushoto) alipata fursa ya kujionea jinsi Shamba la Mfano la Mafunzo-SUA linavyojipambanua katika kutoa elimu ya vitendo kwa wanafunzi wa SUA na wale kutoka nje ya chuo, kwa lengo la kuwaandaa na kuwajengea umahiri katika soko la ajira, ikiwa ni pamoja na kujiajiri au kuajiriwa.
Mbali na utoaji wa elimu ya vitendo kwa wanafunzi, Ndugu Fadhil Maganya alishuhudia uzalishaji bora wa vifaranga vya Sato na Kambale, ambavyo vimekuwa na tija kubwa kwa jamii ya wafugaji na kuendelea kuboresha ukuaji wa Sekta ya Ufugaji Samaki.Shamba hili la Mfano la Mafunzo limekuwa kitovu cha elimu kwa wafugaji na jamii kwa ujumla.Ndugu Fadhil Maganya akisifu kazi nzuri inayofanywa na SUA kwa kusema:
“Elimu hii ya vitendo iendelee kuimarishwa ili kuhakikisha vijana wengi zaidi wanaandaliwa kujiajiri”.
Idara ya Shamba la Mfano la Mafunzo (Model Training Farm-SUA) inawakaribisha watu wote kutembelea na kujifunza Ufugaji wa Samaki Kibiashara kwa njia ya vitendo.
Kwa Maulizo, Tafadhali Wasiliana Na:
Meneja wa Kitengo:
Jina: Stella Genge
Barua Pepe: stella.genge@sua.ac.tz
Simu Na: +255-712-413-590
Afisa Mafunzo (Field Technician):
Jina: Buharata Salum
Barua Pepe: buharata.salum@sua.ac.tz
Simu Na: +255-747-612-361
Kwa Mawasiliano ya Kiofisi tu, Tafadhali Wasiliana Na:
Mkuu wa Idara, Model Training Farm,
Sokoine University of Agriculture,
S.L.P 3001, Chuo Kikuu, Morogoro,
Simu Na: +255753937587
Barua Pepe: newtonk78@sua.ac.tz
CC: dmtf@sua.ac.tz