Idara ya Shamba la Mfano la Mafunzo (Model Training Farm) Ndani ya Viunga vya Tanga

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kinashiriki Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Elimu, Ujuzi na Ubunifu kupitia Ndaki ya Kilimo (College of Agriculture). Ndaki hii inawakilishwa na Idara ya Shamba la Mfano la Mafunzo (Model Training Farm), ambayo ni mojawapo ya Idara sita zilizopo kwenye Ndaki ya Kilimo.

Maadhimisho haya yanafanyika katika viwanja vya Shule ya Sekondari Popatlal, Tanga, kuanzia tarehe 25 hadi 31 Mei 2024.Wakwanza kutoka kushoto ni Mr. Joseph Ruboha, Mkuu wa Idara ya Sayansi za Kilimo na Mhadhiri Kampasi ya Mizengo Pinda-SUA, katikati ni Prof. William Andey Anangisye (Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam) wakiwa na Mtaalam wa Bustani (Mr. Bruno Venance) kutoka Idara ya Shamba la Mfano la Mafunzo (Model Training Farm).

Tunawakaribisha watu wote kwenye banda letu kuja kukutana na wataalam kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) na kupata elimu ya ufugaji vifaranga vya samaki (sato na kambale) kibiashara, upandaji wa malisho, na miche ya matunda.Banda letu litakuwa wazi kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 11 jioni. Sambamba na hili, utapata fursa ya kupata vifaranga bora vya samaki (sato na kambale), miche bora ya matunda, na vipando vya malisho kwa ajili ya ufugaji wa ng’ombe wa maziwa na nyama.Kama upo mbali, unaweza kuweka oda yako sasa ili upate vifaranga vya samaki, vipando vya malisho, na miche ya matunda.

Usikose fursa hii adhimu!

 

Kuweka Oda ya Vifaranga vya Samaki, Tafadhali Wasiliana na: 

Meneja wa Kitengo: 

Jina: Stella Genge

Barua pepe: stella.genge@sua.ac.tz

Simu Na: +255-712-413-590

             AU

Jina: Buharata Salum

Barua pepe: buharata.salum@sua.ac.tz

Simu Na: +255-747-612-361

 

Kuweka Oda ya Miche ya Matunda, Tafadhali Wasiliana na: 

Meneja wa Kitengo: 

Jina: Roman Mfinanga

Barua pepe: roman.mfinanga@sua.ac.tz

Simu Na: +255784684130

          AU

Jina: Buharata Salum

Barua pepe: buharata.salum@sua.ac.tz

Simu Na: +255-747-612-361

 

Kuweka Oda ya Vipando vya Malisho, Tafadhali Wasiliana na: 

Meneja wa Kitengo: 

Jina: Faridi Chamkatwa

Barua pepe: faridi.chamkatwa@sua.ac.tz

Simu Na: +255-712-500-840

                AU

Jina: Buharata Salum

Barua pepe: buharata.salum@sua.ac.tz

Simu Na: +255-747-612-361

Related Posts