FAHAMU KILIMO CHA MIGAZI (MICHIKICHI) KUTOKA SHAMBA LA MFANO LA MAFUNZO SUA

Migazi au Michikichi ni mimea ya aina ya mitende inayostawi vizuri katika udongo wenye rutuba nyingi na usiojaa maji kila wakati. Mimea hii pia hupendelea mvua nyingi. Matunda ya Migazi au Michikichi hutengeneza mafuta yanayoitwa mawese.

Aina za Migazi
Kuna aina kuu tatu za Migazi. Kwanza ni Dura, ambayo ina mbegu kubwa iliyozungukwa na nyama nyembamba. Aina hii hutoa mafuta kidogo ikilinganishwa na nyingine. Pili ni Tenera, ambayo ina mbegu ndogo iliyozungukwa na nyama nyingi, na hivyo hutoa mafuta mengi. Aina ya tatu ni chotara wa Dura na Tenera, ambayo hutoa mafuta kiasi. Shamba la Mfano la Mafunzo SUA lina Migazi aina ya Tenera, ambayo imekuwa chanzo kikubwa cha motisha katika mchakato wa kujifunza.

Kwa taarifa zaidi tembelea HAPA

Related Posts