Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Deo Mwanyika (MB), imetembelea Studio ya Ushonaji Nguo na Bidhaa za Ngozi katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo.
Katika ziara hiyo, kamati imejionea jinsi studio hiyo inavyotengeneza bidhaa mbalimbali na kusaidia wanafunzi kujifunza kwa vitendo. Aidha, wametembelea sehemu mbili kuu za studio hiyo. Sehemu ya kwanza inahusika na ushonaji wa nguo, huku sehemu ya pili ikihusika na utengenezaji wa bidhaa za ngozi kama viatu, mikanda, na mifuko.
Kamati hiyo inayoongozwa na Mheshimiwa Deodatus Philip Mwanyika (Mb) ambaye ni mweneykiti wa kamati hiyo akiongozwa ba Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na wajumbe mbalimbali wa kamati hiyo ambao pia ni wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wametembelea karakana hiyo na kujionea shughuli mbalimbali za karakana hiyo Pamoja na bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na idara hiyo kwa ushirikiano wa walimu na wnafunzi. Pia Mheshimiwa Deodatus amewaasa wanafunzi kutumia karakana hiyo kwa ajili ya kupata ujuzi na uzoefu katika kwenda kuanzisha viwanda vidogovidogo mara watakapo hitimu.
Pia Mkuu wa Idara ya Lishe ya Binadamu na Sayansi ya Mlaji Dr. Hadija Mbwana aliwaeleza wana kamati juu ya shughuli mbalimbali zinazofanyika katika studio hiyo kuwa ni mahususi kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kwa ajili ya wnafunzi wanaosoma Shahada ya Sayansi ya Kaya na Mlaji.