Idara ya Lishe na Sayansi ya Mlaji SUA yakutana na wadau kutoka Sekta mbalimbali nchini kwaajili ya maboresho na ukuzaji wa Mitaala

Idara ya Lishe na Sayansi ya Mlaji SUA yakutana na wadau
kutoka Sekta mbalimbali nchini kwaajili ya maboresho na ukuzaji
wa Mitaala
Na, Ayoub Mwigune
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kupitia Ndaki ya Kilimo, Idara ya
Lishe na Sayansi ya Mlaji imekutana na wadau mbalimbali wakiwemo
waajiri kutoka Sekta mbalimbali wanaohusika moja kwa moja kwenye soko
la ajira ili kuboresha na kukuza Mitaala itakayowawezesha wahitimu
kutoka SUA hasa katika Idara hiyo kuweza kufanya kazi mahali popote
lakini pia kujiajiri wenyewe.
Amesema hayo Dkt. Hadijah Mbwana Mkuu wa Idara ya Lishe na Sayansi
ya Mlaji wakati akizungumza na SUAMEDIA ambapo amesema
wamefanyia kazi Mitaala mitano ambapo katika hiyo miwili ni ya Shahaza
za awali na mingine mitatu ni ya Shahada za juu hivyo wameona vyema
kushirikisha wadau kutoka nje kwakuwa wao ndio wahusika wakuu wa
soko la ajira huko nje na ndio watu pekee wanaofahamu nini ambacho
kinaendelea kwenye soko hilo tofauti na wao ambao kazi yao kubwa kutoa
Mafunzo.
Amesema Mitaala ambayo wanaiboresha sasa inalenga katika kuwafanya
wanafunzi wawe na ujuzi wa kujitegemea wenyewe hivyo kile walichokuwa
wanakihitaji zaidi kutoka kwa wadau hao ni mawazo, michango yao katika
mapendekezo ya Mitaala yao ambayo kwa upande wao walishakaa na
kujadili kile kinachohitajika sehemu iliyobaki ilikuwa ni ya wadau ambao
ndio wahusika wakuu katika kupokea kile tulichokizalisha au kukipatia
Mafunzo.
“Idara yetu ina kozi kubwa mbili ambapo moja ni ya Lishe ya binadamu na
nyingine unahusu mambo ya Sayansi ya Mlaji (Consumer Studies) kwahiyo
tumeleta wadau kutoka kwenye Sekta zote hizo zinazohusika na kozi zetu
moja kwa moja ambazo tunajua zinamchachango mkubwa katika
kuboresha na kuona ni vitu gani vinahitajika kwenye soko la ajira lakini pia
kwenye kukuza ujuzi wa wanafunzi wetu”, alisema Dkt. Hadijah Mbwana
Aidha Dkt. Hadijah Mbwana amesema wanategemea kuwa Maboresho
ambayo waneyafanya yatakuwa kivutio kikubwa kwa wanafunzi wengi zaidi
kwenda SUA hasa katika Idara yao ya Lishe na Sayansi ya Mlaji kwasababu

ni Mitaala ambayo imeangalia sio tu mitazamo ya kitanzania lakini pia
Afrika Mashariki, Afrika pamoja na Dunia kwa ujumla hivyo tunategemea
wanafunzi watakao pitia kwenye Mitaala hiyo wanakuwa na uwezo wa
kujiajiri, kuajiriwa mahali popote duniani vilevile kuajiri wengine.
Kwa upande wake Loitsedi Mlali Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma
za Lishe kwenye Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaala
amesema uboreshaji wa Mitaala SUA vilevile kutunga Mitaala mipya ya
maswala ya huduma za lishe limekuwa jambo jema sana kwakuwa limekuja
kwa wakati sahihi ambao kuna uwekezaji mkubwa sana katika Sekta ya
Afya, ustawi wa jamii na Lishe ambapo wanaenda kwenye huduma bobezi
ikiwemo uboreshwaji wa vituo vya Afya pamoja na vifaa tiba.
Amendelea kwa kusema vitu vyote hivyo ambavyo vimeboreshwa vinahitaji
kuwekwa kwa rasilimali watu wenye ujuzi wa hali ya juu na hilo ni jambo
linalopelekea hata kwenye Vyuo vya elimu ya juu ikiwemo SUA kuweza
kuboresha Mitaala yao iendane na hali ya sasa ya utoaji huduma kwa
wananchi hivyo kupitia warsha hiyo wanaenda kupata Mitaala
itakayozingatia soko la ajira lililopo hivi sasa si tu katika tawala za Mikoa na
mamlaka za serikali za Mitaala bali pia katika Sekta binafsi, Biashara na
uchumi kwa ujumla.
“Sasaivi tunataka vijana ambao wanahitimu katika Vyuo vyetu mbalimbali
nchini wawe na uwezo wa kujitengenezea ajira wao wenyewe lakini vilevile
uwezo wa kuajirika kwenye Sekta binafsi na kuweza kutoa huduma bora za
Sekta za Umma hivyo hayo yote yanahitaji ujuzi mpya ambao unaendana
na Soko la ulimwengu kwaiyo Mitaala hii tunayoiboresha itawasaidia sana
kwenye maeneo hayo lakini pia kwenye mabadiliko makubwa ya Sayansi na
Teknolojia”, alisema Bw. Loitsedi Mlali
Naye Sarah Makweba mwanafunzi wa mwaka wa tatu Kozi ya Sayansi ya
Mlaji SUA amesema mabadiliko hayo ya Mitaala ni mazuri kwakuwa ni
vyema kuangalia namna ya Dunia, utandawazi na teknolojia inavyoenda ili
kuweza kujua zaidi kitu ambacho kinatakiwa kibadilike kutokana na
mabadiliko ya dunia na itakuwa msaada mkubwa sana hasa kwa wanafunzi
ambao watajifunza kwenye Mitaala hiyo inayoboreshwa kwakuwa wataenda
kujifunza kwa uhalisia zaidi.
AM/.
MWISHO

Related Posts

Leave a Reply