Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo, ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Deo Mwanyika (MB), imetembelea Studio ya Ushonaji Nguo na Bidhaa za Ngozi katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo.
Katika ziara hiyo, kamati imejionea jinsi studio hiyo inavyotengeneza bidhaa mbalimbali na kusaidia wanafunzi kujifunza kwa vitendo. Aidha, wametembelea sehemu mbili kuu za studio hiyo. Sehemu ya kwanza inahusika na ushonaji wa nguo, huku sehemu ya pili ikihusika na utengenezaji wa bidhaa za ngozi kama viatu, mikanda, na mifuko.
Kamati hiyo inayoongozwa na Mheshimiwa Deodatus Philip Mwanyika (Mb) ambaye ni mweneykiti wa kamati hiyo akiongozwa ba Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na wajumbe mbalimbali wa kamati hiyo ambao pia ni wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wametembelea karakana hiyo na kujionea shughuli mbalimbali za karakana hiyo Pamoja na bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na idara hiyo kwa ushirikiano wa walimu na wnafunzi. Pia Mheshimiwa Deodatus amewaasa wanafunzi kutumia karakana hiyo kwa ajili ya kupata ujuzi na uzoefu katika kwenda kuanzisha viwanda vidogovidogo mara watakapo hitimu.
Pia Mkuu wa Idara ya Lishe ya Binadamu na Sayansi ya Mlaji Dr. Hadija Mbwana aliwaeleza wana kamati juu ya shughuli mbalimbali zinazofanyika katika studio hiyo kuwa ni mahususi kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo kwa ajili ya wnafunzi wanaosoma Shahada ya Sayansi ya Kaya na Mlaji.
Kuna bunifu mbalimbali za wanafunzi baada ya kupata mafunzo ya nadharia huyawasilisha katika vitendo na kupata bidhaa iliyokamilika iliyozingatia uimara na ubora lakini pia karakana hiyo inatoa pia huduma kwa jamii ya chuo na maeneo mengine Jirani kua mtu yeyote anaweza kununua bidha hizo kwa ajili ya kuongeza pato la idara na chuo kwa ujumla aliongeza Dr Hadijah.
Naye Mary Marcel mfanyakazi wa SUA katika idara hiyo alipata wasaa wa kuwaonyesha wanakamati hao mfano wa vazi la taifa ambalo amelibuni kama sehemu yake ya masomo aliyopata kupitia ufadhili wa HEET kusomea shahada yake ya pili huko Uingereza. Wajumbe walimpongeza kwa hatua hiyo maana Serikali ipo katika mchakato wa kutafuta vazi la Taifa hivyo wamemshauri kupata miongozo katika mamlaka husika ili kazi yake ipate kuonekana na kutambulika.
Wanakamati waliwapongeza walimu na wanafunzi kwa kazi nzuri zinazofanyika katika Studio hiyo na kuwataka waendelee kuwa wabunifu Zaidi ili jamii ipate bidhaa nzuri za nguo na ngozi zinazo tayarishwa hapa hapa nchini ili kuweza kushindana na soko la bidhaa hizo zinazoagizwa kutoka nje ya nchi.
The Department of Human Nutrition and Consumer Studies
The College of Agriculture, Sokoine University of Agriculture
Share this page